Mwimbaji wa nyimbo za Injili Flora Mayala maarufu kama Flora Mbasha
amefungua kesi ya madai dhidi ya mume wake Emmanuel Mbasha kuomba
talaka na kugawana mali walizochuma wakati wakiwa katika ndoa.
Flora alifungua kesi hiyo namba 64/2014 katika mahakama ya hakimu
mkazi Kisutu Jijini Dar es salaam mbele ya hakimu Devotha Kisoka.
Pamoja na maombi hayo Flora aliomba aruhusiwe kuishi na mwanae
Elizabeth Mbasha mwenye miaka 11 na kwamba Mbasha ahusike katika
kumuhudumia mtoto huyo.
Flora alisema ameamua kufanya hivyo kwa sababu ameumizwa,amekua na
msongo wa mawazo na kwamba anahitaji mtu atakayekua mwangalifu naye na
kumsaidia.
Kwa mujibu wa gazeti la habari leo, Alieleza kwamba Mbasha alikua akimfanyia vitendo vya ukatili kwa
kumshambulia kwa kipigo na baadaye kushindwa kutoa huduma na matibabu
anapoumia na pia aliwahi kumtishia kumuua baada ya kuripoti ustawi wa
jamii kuhusu mgogoro huo.
