Mwanafunzi wa Chuo kikuu cha Utabibu Moshi amejifungua mtoto katika choo cha Hospitali ya rufaa KCMC na kisha kumtupa mtoto wake kwenye kasha la takataka.
Tukio hilo ambalo limezua gumzo kubwa mjini Moshi lilitokea juzi asubuhi katika choo kilichopo mapokezi ya wagonjwa waliozidiwa.
Habari kutoka katika hospitali hiyo zinasema mwanafunzi huyo ambaye
kwa sasa jina lake limehifadhiwa ambaye anasoma mwaka wa kwanza anasomea
masomo ya matibabu yamazoezi ya viungo.
Mwanafunzi huyo alifika eneo la
mapokezi akiwa na mwanafunzi mwenzake na akaingia chooni kwa lengo la
kujisaidia na baada ya muda muhudumu wa usafi aliingia na kukuta choo
kimetapakaa damu na baadaye kusikia sauti ya mtoto akilia kutoka kwenye
pipa la taka lililopo ndani ya choo hicho.
Alipochungulia alikutana na mtoto mchanga ambaye alikua hata
hajakatwa kitovu na inasemekana mwanafunzi huyo alikwenda pale baada ya
kusikia ana maumivu ya tumbo na kwa sasa wanamshikilia na uongozi
wahospitali kwa uchunguzi zaidi.