MAKUBWA...AWAFYATULIA RISASI WATU WAWILI KWA MADAI WANAMPIGIA KELELE KWENYE HARUSI HUKO DAR

Mtu mmoja amewafyatulia risasi watu wawili na kupelekea mmoja kufariki na mwingine kujeruhiwa akiwalalamikia kumpigia kelele wakati watu hao walipokuwa kwenye mkesha wa harusi Dar.

Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Kipolisi Ilala, David Mwambunga amethibitisha kutokea kwa tukio hilo japo amekataa kuzungumzia suala hilo kwa kuwa yeye sio msemaji rasmi.

Majeruhi wa tukio hilo, Goodluck Madaraka amesema siku ya tukio walikuwa wakicheza muziki majira ya saa tano usiku ndipo jirani yao Lucas Muhabe alitoka na panga akiwafukuza kwamba wanampigia kelele, muda mfupi baadaye akarudi na bastola na kuanza kupiga risasi hewani ambapo moja ilimpata mpita njia Mahamudu Muhasi kichwani, akafariki.

Kaka wa marehemu amesema mdogo wake alikuwa akipita njia tu jirani na ilipo sherehe hiyo hivyo ameuawa lakini hakuhusika.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo