Mtoto
mmoja mwenye umri wa miaka Sita amefariki dunia baada ya kutupwa na
bibi yake nje ya basi kupitia dirishani wakati basi likiwa katika mwendo
wa kasi mkoani Singida.
Bi. Lawaridi Saidi aliyemtupa mtoto huyo
Katika
hali isiyo kuwa ya kawaida mama moja aliye kuwa akisafiri na mtoto
wake mmoja na wajukuu zake wawili, aliamua kumtupa mjukuu wake wa miaka
sita dirishani huku basi likiwa katika mwendo kasi na kusababisha kifo
chake baada ya kufikishwa katika hospitali ya mkoa wa Singida.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa jeshi la polisi
mkoani Singida ACP Thobias Sedoyeka, amesema mama huyo aliye tambulika
kwa jina la Lawaridi Saidi mweye umri wa miaka 46 aliyekuwa akisafiri na
basi namba T 981 ALS kampuni ya Salumu Clasc lilokuwa likitokea
Dar-es-salaam na kuelekea Kigoma.

Amesema alipofika katika kijiji cha Iguguno wilaya ya Mkalama siku ya
tarehe 18/12/2014 saa 2 usiku alimtupa mjukuu wake Mayasa meshaki
dirisani huku basi likiwa katika mwendo kasi.
Kwa upande wake mganga wa zamu katika hospitali ya mkoa wa Singida
Dkt Adamu Hussein amesema walimpokea mtoto huyo akiwa katika hali mbaya
akiwa hapumui vizuri na damu kutoka katika masikio,baada ya kumpatia
matibabu alilazwa na siku ya pili alifariki kutokana na kupasuka kwa
fuvu la kichwa.
Akieleza jinsi alivyo mtupa mjukuu wake huku basi likiwa katika
mwendo kasi Lawaridi Saidi ambaye ni mkazi wa Kongowe jijini
Dar-es-salaam amesema baada ya kuamka akiwa katika hali ya usingizi
alijikuta akimchukuwa mjukuu wake Mayasa na kumtupa dirishani na
hatimaye abiria wakaanza kumpiga na kuamuru basi lisimame na kumtafuta
mtoto huyo.