Wananchi wakiwa eneo la Sogea, Tunduma ilipotokea ajali ya basi na Coaster.
WATU
kadhaa wamejeruhiwa katika ajali iliyolihusisha Basi la Shalom Express
lililokuwa likitokea Sumbawanga - Mbeya lililogonga Coaster iliyokuwa
inatokea Mbeya- Tunduma eneo la Sogea, Tunduma jioni ya leo. Coster
lilikuwa likijaribu ku-overtake lori ndipo lilipogongwa na basi hilo.
Idadi kamili ya majeruhi wa ajali hiyo bado haijafahamika.
