Zaidi ya nyumba hamsini na moja zinazo kadiriwa kuwa na wakazi zaidi
ya miambili, katika Manispaa ya Singida, zimebomolewa na Mvua kubwa ya
mawe iliyonyesha ikiambatana na upepo mkali.
Mvua hiyo iliyoanza kunyesha majira ya jioni imesababisha hasara
kubwa kwa wakazi wa manispaa hiyo ambapo, mpaka sasa nyumba hamsini na
moja zimeharibiwa ikiwemo Nyumba za watu binafsi na Madarasa ya
Misikiti.
Mkuu wa Wilaya Qeen Mlozi amesema …”Serikali
ya Mkoa kwa kweli mvua iliyonyesha jana takribani dakika kumi na tano
paka ishirini ilikuwa mvua kubwa ya mawe na upepo mkal, ambayo
imesababisha nyumba nyingi za mjini Singida zimeharibiwa na upepo, paka
sasa wakati wataalam wanaendelea jumla ya nyumba hamsini na moja ,
zimeanguka, zimeharibiwa, zimeezuliwa na upepo”
Ally Sanga Mkazi wa Singida amesema… “Imekuja
mvua tuu mida ya jioni hii imedumu kama dakika 15 hivi alafu umekuja
upepo mkali na mawe, ndio imesababisha madhara yote ambayo mnayaona
imeangusha Nyumba, Miti, Nyaya za umeme zimekatika yani watu wana hali
mbaya sana”
Wakazi wa Manispaa hiyo wamesema Mvua iliyonyesha haijawahi kutokea
pamoja na kunyesha kwa muda mfupi, lakini imeleta madhara makubwa sana
na kulalamikia Manispaa ya Singida kwa kutokutengeneza vizuri
miundombinu ya maji na kusababisha Nyumba nyingi kubomoka.