Waziri wa Uchukuzi Dr. Harrison Mwakyembe amekabidhiwa Ripoti ya kamati iliyoundwa kutathmini na kutoa mapendekezo hatua ya kuchukua ili kupunguza ajali za barabarani.
Kamati hiyo iliyoundwa na watu 14
imebaini changamoto zinazopelekea ajali hizo kuwa ni pamoja na ratiba za
mabasi zinazotolewa na SUMATRA kutozingatiwa pamoja na utaratibu mbovu
wa utoaji wa leseni.
Akizungumza wakati wa kupokea Ripoti hiyo Mwakyembe amesema; “…
Ajali nchini zinasababishwa na Mwendokasi na uendeshaji hatarishi au
kwa maneno mengine uzembe. Waziri Gaudensia Kabaka yeye tayari Wizara
yake imefanya kazi kubwa kweli, wamekuja wao na ratiba kabisa ya ukaguzi
wa kampuni zote za mabasi na malori, ni ratiba ya miezi miwili
kuchunguza mikataba ya kazi kwa upande wa madereva kwa mwezi Desemba na
Januari, inasubiri tu Waziri aseme tunaanza tarehe fulani.
Kwa hiyo
siyo tu mikataba ya kazi inaangaliwa, itaangaliwa mpaka na michango ya
mwajiri au waajiri na waajiriwa kwenda kwenye mifuko ya Hifadhi ya
Jamii…”– Mwakyembe.
ITV imeripoti kuhusu taarifa hiyo na hapa nimekuwekea sauti niliyoirekodi, unaweza kuisikiliza kwa kubonyeza play.