Mwanamke mmoja nchini China ambaye ni mjamzito amehukumiwa kifungo
cha maisha huku mume wake akihukumiwa adhabu ya kifo baada ya
kushirikiana kumbaka na kisha kumuua msichana wa miaka17.
Mwanamke huyo ambaye anajulikana kwa jina la Tan Beibei alifanya
kitendo hicho baada ya msichana huyo kumsaidia alipoanguka barabarani
ambapo alimpeleka hadi nyumbani kwake na badala ya kumshukuru waliamua
kumfanyia kitendo hicho cha akishirikiana na mumewe kisha kumuua na
kuamua kumzika.
Mahakama ya Heillojiang ya nchini humo imesema kuwa imewafungulia
mashtaka ya kuua,kubaka pamoja na kushambulia baada ya mwanamke huyo
kujifanya ni mgonjwa na kushirikiana na mumewe kumfanyia binti huyo
kitendo hicho cha kudhalilisha kisa wivu kwa madai alikua akitembea na
mumewe.
Mahakama ya juu ilikataa kuwapunguzia adhabu wawili hao baada ya
kukata rufaa kwa madai kesi hiyo ni kubwa na haina dhamana yoyote.
Kwa mujibu wa mashuhuda msichana huyo aliyejulikana kwa jina la Hu
alikua akipita barabarani ndipo mama huyo alipomwomba msaada wa
kumpeleka nyumbani kwake baada ya kuanguka na msichana huyo kutii lakini
alipofika alikutana na maswaiba hayo.
Inaelezwa kuwa baada ya kufika mume wa
mwanamke huyo alimpa msichana huyo maziwa ya mtindi na baadaye kuanza
kumfanyia kitendo hicho akishirikiana na mkewe lakini hata hivyo
hawakufanikiwa kwani binti huyo aliweza kuwazidi nguvu na walipoona
imeshindikana walichukua blanketi na kumziba nalo usoni hadi alipofariki
dunia na kuamua kumzika.
Katika utetezi wa mwanamke huyo mahakamani hapo alisema aliamua kufanya kitendo hicho kwa sababu binti huyo alikua akitembea na mume wake.
Historia inaonyesha wawili hao walishawahi kuwa na kesi mbalimbali
kiwemo ya kutaka kumbaka rafiki wa mtoto wao wa kike ambaye alikua
akisoma naye darasa moja.