Mwanamke mmoja Swaumu Aboubakari mwenye miaka24 mkazi wa Keko Jijini
Dar es salaam ambaye ni mjamzito amenusurika kufa baada kupigwa na vitu
vyenye ncha kali na mzazi mwenzake kutokana na ugomvi wa kifamilia.
Akizungumza kwa shida katika wodi alikolazwa Hospitali ya
Mwananyamala alisema ameishi na mzazi mwenzake kwa takribani miaka
mitano huku ndoa yao ikitawaliwa na migogoro kila wakati.
Alisema baada ya Mateso kuongezeka alichukua uamuzi wa kurudi
nyumbani kwa wazazi wake akiwa na mtoto wake mwenye umri wa mwaka mmoja
huku akiwa na ujauzito mwingine.
Alisema juzi usiku alitoka Keko kwenda Tandale kwa mzazi mwenzake kwa
ajili ya kuomba fedha za matumizi lakini akiwa ndani ya nyumba yake
mwanaume huyo alitoka sebuleni na kumchukua kwa nguvu mtoto na kwenda
kumlaza chumbani na aliporudi alianzisha ugomvi akishirikiana na ndugu
zake akimuhumu mwanamke huyo kuwa mimba si yake.
“Mume wangu bila hata huruma akishirikiana na ndugu zake walinipiga
kwa kutumia waya,rungu,fimbo na chuma,sehemu mbalimbali za mwili na
nimejaa vidonga kama mnavyoona”alisema Mwanamke huyo.