Watu 11 wamekufa papo hapo na wengine 25 kujeruhiwa baada ya basi
dogo aina ya Coaster kugongana uso kwa uso na lori la mizigo aina ya
scania katika kijiji cha Mkanyageni Wilaya ya Muheza,Mkoani Tanga.
Ajali hiyo ilitokea jana saa11 asubuhi wakati basi hilo lili[okua
linatoka Tanga kwenda Lushoto na Lori hilo likitokea Lushoto
kwendaTanga.
Kaimu Mganga mkuu wa Wilaya Peter Mwankai alisema miili ya marehemu
hao imehifadhiwa katika hospitali teule ya Muheza na tayari maiti saba
zimetambuliwa na ndugu zao.
Alisema majeruhi 22 wanaendelea vizuri na wana endelea kupatiwa matatibabu katika hospitalihiyo chini ya uangalizi maalum.
JIUNGE NA EDMO BLOG SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube
Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi