Mwanaume mmoja Nyakibura Kina mwenye miaka 49 amemuua mkewe wa pili
Tano Matuma kwa kumpiga kisha kumnyonga kwa kutumia mikono yake.
Hata hivyo mwanaume huyo baada ya kumaliza kitendo hicho aliichukua
maiti hiyo na kuificha chini ya uvungu wa kitanda chake na kwenda katika
nyumba nyingine iliyopo jirani kisha kujinyonga kwa kutumia kamba ya
katani.
Mwenyekiti wa kijiji cha Sirosi Mara Alexender Makike alisema
waligundua tukio hio jana asubuhi baada ya mtoto wa marehemu kuamka na
kuona mwili wa mama yake ukiwa uvunguni mwa kitanda.
Alisema baada ya mtoto huyo kuona alianza kulia na kuomba msaada
ambapo majirani walipofika walikuta maiti ya mwanamke huyo ikiwa chini
ya kitanda na wakati wakihamaki waliona mwili wa mwanaume huyo ukiwa
katika nyumba nyingine ambayo ilikua bado haijaisha.