Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali katika Bunge la Jamumuhi ya Muungano wa Tanzania, imewasilisha ripoti ya uchunguzi wa kashfa ya IPTL na kuhusisha uchotwaji wa shilingi bilioni 306 za kitanzania.
Pamoja na kuwepo tetesi za pingamizi ya mahakama kuzuia kusomwa kwa
ripoti hiyo Bungeni, Mwenyeti wa kamati Zitto Kabwe alisoma ripoti na
kulithibitishia Bunge hilo kwamba viongozi na wafanyakazi wa Serikali,
wafanyabiashara, viongozi na taasisi za dini, mabenki na watu binafsi
wanahusika kufanya ufisadi huo.
Mwenyekiti Kabwe pia ameliambia Bunge kwamba, kwa kutumia njia zisizo
halali, watu hao walifanikiwa kutoa fedha kutoka akaunti ya Tegeta
Escrow ndani ya Benki Kuu ya Tanzania, iliyofunguliwa baada ya mgogoro
na kapuni ya ufuaji umeme ya IPTL na Tanesco.
Naye Makamu mwenyekiti wa kamati hiyo ya Bunge Deo Filikunjombe, akisoma
sehemu ya pili ya ripoti hiyo ya mapendekezo ya kamati, amesema wale
wote waliohusika wawajibishwe.
Ameongoza kuwa kuwajibishwa huko ni pamoja na kufilisiwa kwa wahusika
kwa mali zao kupigwa mnada na ikiwezekana hata zile za nje ya nchi.
Pia Filikunjombe, alitaka viongozi wote wa Serikali waliotajwa katika
ufisadi huo wawajibike pamoja na watumishi wa Serikali kufukuzwa kazi.
Bunge litaendelea leo saa tatu asubuhi na inatazamiwa mjadala mkali kuzuka na baadhi ya
viongozi wa Serikali waliotajwa kujiuzulu.
KUPATA RIPOTI KAMILI YA PAC KUHUSU ESCROW
<< BONYEZA HAPA>>
Ingia hapo juu kuipakua Ripoti nzima
KUPATA RIPOTI KAMILI YA PAC KUHUSU ESCROW
<< BONYEZA HAPA>>
Ingia hapo juu kuipakua Ripoti nzima