Jopo la majaji watatu wa mahakama kuu kanda ya Dar es Salaam chini ya
jaji Radhia Sheikhe limezuia mjadala wa ripoti ya mdhibiti na mkaguzi
mkuu wa serikali kuhusu akaunti ya Tegeta Escrow hadi hapo hoja ya
msingi ambayo ipo mahakamani itakapofanyiwa kazi.
Jopo hilo lililokuwa likiongozwa na Mh Radhia Sheikhe wameagiza
kutofanyika kwa mjadala wotote kuhusu ripoti ya CAG huko bungeni na
kuongeza kuwa majadiliano hayo yanaweza kufanyika baada ya shauri la
msingi kupatiwa ufumbuzi.
Awali
akizungumza na mwandishi wetu, mwanasheria wa IPTLl wakili Joseph
Makandege amesema wamefikisha shauri hilo namba 50 katika mahakama hiyo
wakitaka vifanyike vitu viwili kwanza kupata tafsiri sahihi ya kisheria
kuwa kama kitendo kilichofanywana ofisi ya CAG kufanya ukaguzi katika
akaunt za Escrow kama ni sahihi akaongeza kuwa wao wanachoamini ni kuwa
kwa sababu jambo hilo lilikuwa limekwisha amuliwa kisheria mahakamani
na kutolewa hukumu kulikuwa hakuna haja tena ya bunge kuagiza
uchunguzi ufanyike.
Aidha mwanasheria huyo alisema kuwa siyo kwamba hawataki jambo
hilo kujadiliwa bali wanataka taratibu zifuatwe ili kuweza kufikia
mwafaka wa kina katika jambo hilo.
Mwanaasheria huyo aliongeza kuwa mbali na kupata tafsiri hiyo ya kisheria pia wanaiomba mahakama kulitaka bunge kusitisha mpango wake wa kujadili tarifa ya CAG hadi tafsiri ya kina ipatikane.
Mwanaasheria huyo aliongeza kuwa mbali na kupata tafsiri hiyo ya kisheria pia wanaiomba mahakama kulitaka bunge kusitisha mpango wake wa kujadili tarifa ya CAG hadi tafsiri ya kina ipatikane.
Mwanasheria huyo pia amesema kuwa wao wanaona kama likijadiliwa
haki haitaweza kutendeka kwa sababu wao kama IPTL hawana mwakilishi
bungeni na hivyo maamuzi yatafanyika upande mmoja.
Kwa upande wa jopo la wanasheria wa serikali wakiongozwana Obadia
Kaimela wameiomba Mahakama kuwapa muda wa kuweza kuwasiliana na baadhi
ya watu ama taasisi zinazohusishwa na jambo hilo ili kuweza kupata muda
wa kutosha kutoa utetezi wao.
Kutokana na hali hiyo imeamuliwa kuwa bada ya kukamilika kwa taribu
zote za kesi ya msingi ikiwemo uwasilishwaji wa viapo, kesi ya msingi
itanza kusikilizwa Desemba 2 mwaka huu.
Hata hivyo Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali ameendelea kusisitiza kuwa kesho (26/11/2014) atatoa Ripoti Bungeni kuhusu upotevu wa pesa za ESCROW.
Zitto ametoa taarifa ifuatayo akinukuu Ibara ya 100 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977.
“Madaraka na Haki za Bunge
100.-(1) Kutakuwa na Uhuru wa mawazo, majadiliano na utaratibu katika Bunge na Uhuru huo hautavunjwa wala kuhojiwa na chombo chochote katika Jamhuri ya Muungano, au katika Mahakama au mahali penginepo nje ya Bunge.
"Kesho tarehe 26 Novemba 2014 Bunge litajadii Taarifa ya PAC kuhusu uchotwaji wa Fedha kutoka akaunti ya #TegetaEscrow “