Hakuna wa Kuzuia Escrow Isijadiliwe Bungeni - Anna Makinda


Kufuatia  Taarifa za  kujadiliwa kwa suala la  ufisadi katika akaunti ya Tegeta Escrow kupelekwa mahakamani ili lisijadiliwe na Bunge, Spika wa Bunge Bi. Anna Makinda amesema hakuna Muhimili utakaoweza kuingilia shughuli za bunge.
 
Akitoa Muongozo wake Baada ya Mbunge wa Bariadi Mashariki Mh. John Cheyo kutaka kujua ni hatua gani zitachukuliwa na Bunge dhidi ya suala hilo kufikishwa mahakamani, Spika Makinda amesema kinga za Bunge ziko wazi na hakuna mtu anayeweza kuwashtaki ili wasifanye kazi yao.
 
Tamko hilo limetolewa na Spika Makinda baada ya maafisa wanao jitambulisha kuiwakilisha PAP kwenda mahakama kuu ya DSM kufungua shauri la kuzuia suala la Escrow kujadiliwa na Bunge.
 
Maafisa hao wa PAP wamefungua shauri namba 50 ya 2014 mahakama kuu kanda ya DSM ambapo wanamshitaki Waziri Mkuu, Spika, CAG na Katibu wa Bunge.
 
Hoja za PAP dhidi ya watu hao wanaoshitakiwa ni kushindwa kutekeleza majukumu yao kwa wakati, kudai faida ya mahakama kwa jambo lililokwisha kutolewa hukumu pia wanadai kukaguliwa na CAG na kuzuia mjadala wowote wa suala hilo hadi ufafanuzi wa mahakama utakapo tolewa.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo