Shirika
la Viwango Tanzania (TBS) jana liliteketeza kondomu feki aina ya Mood
vipande 601,100 vyenye thamani ya Sh. milioni 29.7 ambazo zimebainika
kutengenezwa India.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam baada ya zoezi hilo lililofanyika katika eneo la
Pugu Dampo, Ofisa Ubora kutoka TBS, Athuman Kisumo, alisema kondomu hizo
ziliteketezwa baada ya kuwasili nchini na kubainika hazina ubora na
hazifai kwa matumizi.
Vipimo vya maabara vimethibitisha bidhaa hiyo imekosa ujazo wa hewa pamoja na matundu ya maji, alisema.
“Tutaendelea
na ukaguzi wetu kila mara ili tuweze kubaini bidhaa hafifu, lengo la
kufanya hivyo ni kuhakikisha mlaji analindwa na anakuwa salama wakati
wote,” alisema.
Kwa
mujibu wa ofisa huyu, kondomu hizo ziliagizwa na kiwanda cha Planet
Phamaceutical kwa ajili ya kuzisambaza kwenye maduka Ya jumla na
rejareja ndipo ilipobainika hazina viwango vinavyopendekezwa na TBS.
Aliongeza
kuwa kwa mujibu wa vipimo vya maabara, bidhaa hiyo inapasuka haraka na
haiwezi kuhimili mikiki, hivyo ni rahisi mtu kupata ujauzito asio
tegemea au kupata maambukizi ya Ukwimu na magonjwa ya zinaa.
Afisa
Uhusiano wa Kiwanda cha Planet Phamaceutical, Richard Muyombo, alisema
bidhaa hiyo waliagiza Agosti mwaka jana na kwamba wanajihusisha na
uuzaji wa dawa na vifaa tiba.
Alisema
TBS inatakiwa kuhakikisha inakuwa na mawakala wao ili kuzuia mizigo
isiingie nchini na siyo kusubiri hadi ifikishwe nchini na kuteketezwa.