WAZIRI CHIKAWE HAJACHOKA NA SIASA, ATANGAZA KUTETEA JIMBO LAKE

http://www.fullshangweblog.com/wp-content/uploads/2014/10/PIX-15.jpgNa Felix Mwagara, Nachingwea.

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo  la Nachingwea, Mathias Chikawe ametangaza rasmi kuwa atagombea tena  katika nafasi ya ubunge kupitia CCM katika uchaguzi Mkuu ujao na  kulitetea jimbo lake. 

Alisema hayo juzi alipokuwa akizungumza na  wananchi pamoja na viongozi wa CCM wa Wilaya na Kata ya Mtua, wilayani  Nachingwea katika sherehe ya kuwapokea viongozi na wanachama wapya wa  Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) waliojiunga na CCM wilayani  humo. 

Waziri Chikawe alisema wananchi wake bado wanamuhitaji kwa hiyo  hawezi kuacha kugombea nafasi hiyo kwani wazee na wananchi mbalimbali  katika Kata zote alizokuwa akipita kufanya mazungumzo nao wanamuomba  agombee tena nafasi hiyo. 

“Wakati nikiingia ubunge mwaka 2005 katika jimbo hili kulikuwa  hakuna lami na barabara nyingi za kwenda vijijini zilikuwa hazipitiki na pia maji yalikuwa shida lakini sasa barabara za lami mjini Nachingwea  zimejengwa, maji yanapatikana tena yasio na chumvi, barabara vijijini  zinapitika kwa kuwa zimechongwa vizuri kwa kuwawezesha wakulima  kupitisha mazao yao,” alisema Chikawe huku akishangiliwa na mamia ya  wananchi waliofurika katika sherehe hiyo. 

Picha/Story na Felix Mwagara.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo