Waziri
wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akimsalimia mmoja wa wagonjwa
waliofuata huduma katika zahanati ya Ngarenanyuki wilayani Arumeru
,juzi alipoitembelea baada ya Mbunge wa jimbo hilo kumlalamikia kuhusu
tozo ya ushuru wa magari na wagonjwa wanaopita katikA Hifadhi ya Taifa
ta Arusha ili kupata huduma katika hospitali hiyo. Waziri Nyalandu
aliamuru wananchi wanaohitaji kupata tiba katika zahanati hiyo kupita
bure hifadhini. Mbunge
wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari akimtaarifu Waziri wa Maliasili na
Utalii Lazaro Nyalandu juu ya adha wanayopata wananchi wa jimbo lake
wakati wakiiingia katika Zahanati ya tiba za Asili cha Ngarenanyuki
mkoani Arusha juzi , kutokana na tozo la pesa kupitia hifadhi ya Taifa
ya Arusha. Waziri Nyalandu aliamuru wananchi wanaohitaji kupata tiba
katika zahanati hiyo kupita bure hifadhini. Waziri
wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akiwa na Mbunge wa Siha ambaye
ni Naibu waziri wa Serikali za Mitaa, Aggrey Mwanri wakikagua kitalu cha
miti katika shamba la mitiulioko wilayani humo juzi. Waziri Nyalandu
aliruhusu nguzo nza umeme kupita katika msitu huo ili kuwezesha wananchi
wa wilaya hiyo kupata umeme n akuondoa mgogoro uliozuia mradi huo kwa
muda mrefu.
Naibu
waziri wa Serikali za Mitaa, Aggrey Mwanri akiwa na wataalamu na Waziri
wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu wakikagua msitu wa Siha mkoani
Kilimanjaro alipotembelea juzi . Waziri Nyalandu aliruhusu nguzo nza
umeme kupita katika msitu huo ili kuwezesha wananchi wa wilaya hiyo
kupata umeme.
……………………………………………………………..
Serikali imepiga marufuku ukataji
wa miti nchini hata kama ikiwa mtu amepanda nyumbani kwake anatakiwa
kuomba kibali kwajili ya kukata mti huo.
Akizungumza wilayani Siha juzi
,Waziri wa Maliasili na Utalii , Lazaro Nyalandu amesema kwamba Tanzania
inawez a kuwa jangwa baada ya miaka 15 kutokana na uvunaji mbaya wa
bidhaa za miti unaofanyika nchini .
“Tukiendelea kukata miti kma hivi
tutakuwa tunatengeneza janga la kitaifa kwa hiyo kwa sasa naomba niseme
rasmi kuwa hakuna mtu anaruhusiwa kukata miti au mti hata kama ameupanda
nyumbani kwake, ni lazima aombe kibali kwa maafisa wa misitu.
Tunatakiwa kushiriki kwa pamoja katika kutunza mazingira yetu” alisema.
Nyalandu alisema kasi ya ukataji
miti nchini imekuwa kuubwa kwa sasa kutokana na kuongezeka kwa idadi ya
watu na kuwa kwa mwaka mmoja pekee hekta 350,000 hukatwa huku kikiwa
hakuna jitihada za kurejesha iliyoondolewa.
“Kwa kaddri siku zinavyozidi
kwenda na watu kuongezeka baada ya miaka kumi misitu itakuwa inavunwa kw
azaidi ya hekta 850,000 nchini kwa mwaka, hii ni hatari kubwa, lazima
tufanye jitihada zaidi kukomesha tatizo hili”.
Aliwaagiza wakuu wa wilaya za
Arusha na kilimanjaro kuunda timu ili kuandaa hadidu za rejea kwa ajili
ya kupatia kikosi kazi ambacho kitaandaas andiko kw ajili ya kuanzisha
mfuko huo.
Mtendaji Mkuu wa wakala wa misditu
(TFS) Juma Mgoo alisema kwamba misitu ilianza kutunzwa mtokea enzi za
wakoloni lakini tatizio kubwa linalotokea kw asasa ni watu wengi
kuivamia kutokana na mahitaji ya nishati na uchomaji wa misitu.
Alisema kwamba kwa msitu wa asili
kawaida huwa na mita 30 za ujazo wakati kwa upande wa misitu ya
kuoandwea huwa wna ujazo wa zaidi ya mira za ujazo 400 hadi 600 kitu
ambacho alishauri umuhimu w akupanda miti zaidi ili iweze kukabiliana
na ongezeko la mahitaji na kuokoa misitu iliyopo.
Waziri Nyalandu alitoa maagizo ya
kuruhusu nguzio za umeme kupita katika msitu wa wilayani Siha ili
kufanywa wananchi waweze kupata nishati ya umeme ili kuokoa matumizi ya
kuni kama nishati na kulinda misitu.
“Umemem ni nishati mbadala badala
ya kuni na mkaa kwa hiyo napenda kuwaeleza kwamba ni bora miti michache
ikatwe ili pupisha nguzi za umeme ili wananchi wakipata nishati hiyo
waache kutumia kuni na kuharibu misitu na kutumia umeme kama nishati
mbadala” alisema.