Taarifa kutoka Australia zinasema mtu mmoja amewekwa katika uangalizi
maalumu akifanyiwa vipimo ambapo taarifa za awali zimesema kuwa mgonjwa
huyo ana homa na dalili za maambukizi ya Ebola.
Mtu huyo mwenye umri wa miaka 18 amewasili Australia akitokea Guinea
siku 11 zilizopita akiwa ameongozana na ndugu zake 8 ambapo walimuweka
katika karantini ya nyumbani na baadaye hali yake ilibadilika.
Majibu ya awali ya uchunguzi wa vipimo yanatarajiwa kutoka mapema
Jumatatu, na mgoonjwa huyo atafanyiwa vipimo vingine ndani ya siku 3.
Majibu yakionesha ana maambukizi ya ugonjwa huo Australia itakuwa
nchi ya tisa kupatikana na mgonjwa wa Ebola tangu iliporipotiwa kuzuka
kwa ugonjwa huo mwezi Machi mwaka huu nchi za Afrika Magharibi, na pia
atakuwa ni mgonjwa wa kwanza kuumwa ugonjwa huo Australia.