Waziri
Mkuu Mizengo Pinda (kushoto) akimkabidhi mfano wa hundi ya shilingi
milioni tano Dk. Maria Kamm aliyetwaa Tuzo ya Mwanamke Bora wa Mwaka
2013/2014 ndani ya Ukumbi wa African Dreams uliopo Area D, Dodoma jana
usiku.
Waziri Mkuu akimkabidhi tuzo, Anna Margareth Abdallah, kwa niaba ya mshindi wa pili ambaye ni Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Asha-Rose Migiro.
Waziri Mkuu akimkabidhi tuzo Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi Profesa Anna Tibaijuka aliyeibuka mshindi wa tatu katika tuzo hizo.
Mbunge
wa Same Mashariki (CCM) Anne Kilango Malecela, akipokea tuzo kutoka kwa
Waziri Mkuu Mizengo Pinda baada ya kushika nafasi ya nne.
Dk.
Maria Kamm akipokea tuzo kutoka kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda baada ya
kuibuka kinara wa Tuzo ya Mwanamke Bora wa Mwaka 2013/14.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda (katikati) katika picha ya pamoja na washindi walioingia nne Bora. Kutoka kushoto; Anna Abdallah aliyechukuwa tuzo kwa niana ya Asha-Rose Migiro, Anne Kilango Malecela ,Dk. Maria Kamm na Profesa Anna Tibaijuka.
Waziri Mkuu akiwa katika picha ya pamoja na washindi, waandaaji wa tuzo hizo kutoka Global Publishers Ltd.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Global Publishers Ltd, Eric Shigongo, akitoa hotuba fupi
wakati wa utoaji tuzo kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi ambaye alikuwa
Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
(PICHA ZOTE NA RICHARD BUKOS / GPL, DODOMA)