sokwe mmoja ambaye amepewa jina la
Zaire, ambaye anafugwa katika bustani moja ya wanyama London, Uingereza
amesherehekea siku yake ya kuzaliwa ambapo ametimiza miaka 40.
Na kama haitoshi, party yake ilikuwa poa
kama ambazo huwa tumezoea kufanya binadamu, ametengenezewa keki ya
nguvu katika sherehe hiyo na moja ya mabingwa wa kutengeneza keki za
sherehe, Richard Burr.
Unaambiwa sokwe huyu anapendelea vitu
kama jelly zisizo na sukari, apples, na karoti hivyo mwandaaji wa keki
alijikuta na jukumu la kuhakikisha anamuandalia keki itakayomfurahisha
Zaire.
Hizi ni picha za Sokwe huyo akijiachia na keki akisherehekea.