Viongozi wa vyama vinavyounda UKAWA (CHADEMA, CUF, NCCR Mageuzi na
NLD) wamesaini makubaliano ya kushirikiana katika chaguzi zote ikiwemo uchaguzi mkuu wa Rais na Wabunge unaotarajiwa
kufanyika mapema mwakani.
Akisoma makubaliano hayo kwa niaba ya makatibu wakuu wa vyama
hivyo, katibu mkuu wa Chadema Dokta Wilbrod Slaa amesema chini ya
makubaliano hayo vyama hicho vimekubaliana kuuwisha sera za vyama hivyo
kwa kuchukua yale yanayofanana ili kuwa na kauli zinazofanana
wanapozungumza na wananchi, pamoja na kushirikiana katika mchakato wa
kuelimisha wananchi kupiga kura ya hapa kwa katiba mpya
inayopendekezwa.
Wakizungumza baada ya kusaini hati ya makubaliano, mwenyekiti wa
chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema amewatoa wito kwa viongozi wa
chama hicho katika mikoa kutokwamisha mipango ya Ukawa kwa kuwa ni
mpango wa mungu na kuwataka vingozi wa vyama vinavyounda umoja huo
kuhacha kukaa maofisi kwenda kwa wananchi kuendeleza mapambano, huku
mwenyekiti wa CUF taifa Prof Ibrahimu Lipumba amewataka wananchi
kutopiga kura ya ndiyo kwa katiba inayopendekezwa ili kuwezesha rasimali
za nchi zitumike kwa faida ya wananchi wote.
Aidha kwa upande wa mwenyekiti wa chama cha NCCR- Mageuzi mhandisi
James Mbatia amewataka viongozi wa vyama hivyo katika mikoa kukaa
kungalia wagombea wanaokubalika bila ya kujali chama na kuacha
kulalamika ili kuwasaidia watanzania kupata maendeleo kupitia rasilimali
zao, huku mwenyekiti wa chama cha NLD Dkt Emmanul Makaidi akisisitiza
umuhimu wa kujenga umoja utakaosadia kuleta mageuzi yatakayoleta mchango
mkubwa kiuchumi.
Makubaliano yamefanyika katika viwanja vya Jangwani jiji Dar es
Salaam na kushuhudiwa na maelfu ya wanachama, wapenzi na mashabiki wa
vyama hivyo walikuwa wamebeba mabango yenye ujumbe mbalimbali ambao
wengie wao wameingia kwa maandamano kutoka katika maeneo mbalimbali ya
jiji la Dar es Salaam.
Viongozi
wa juu wa vyama vinne vya siasa nchini Tanzania vimeingia makubaliano
ya ushirikiano wa shughuli mbalimbali za siasa hii leo na miongoni mwa
mambo hayo ni kusimamisha wagombea wa pamoja katika uchaguzi wa Serikali
za Mtaa na Uchaguzi Mkuu wa wabunge, madiwani, wawakilishi na Rais
2015. Kutoka kushoto ni James Mbatia wa NCCR-MAGEUZI, Prof Ibrahim
Lpumba wa chama cha Wananchi CUF, Freeman Mbowe wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Dk. Emmanuel makaidi wa NLD
wakionesha hati yao ya makubaliano waliyoisaini jana katika viwanja vya
Jangwani Dar es Salaam leo.
Viongozi hao wakishangilia kuzaliwa kwa ushirikiano huo huku makatibu wao wakiwa wameketi.
Wafuasi,
wanachama, wa vyama vya siasa vinavyounda ukawa wakifuatilia mkutano
huo ambao ulianza kwa kuimba wimbo wa Taifa huku wanachama hao wakiwa
wamekaa jambo ambalo lilielezwa na viongozi wao kuwa uzalendo ni ndani
ya moyo. Chini ndio mambo waliyokubaliana.