Jeshi
la polisi Zanzibar limefanikiwa kumkamata mtu mmoja akiwa na mabomu
manne ya kivita ambayo yanasadikiwa ni miongoni mwa mabomu yanayotumika
katika vitendo vya uhalifu yaliyotokea sehemu mbali mbali nchini.
Kamishna wa jeshi la polisi Zanzibar CP Hamdani Omar Makame
amethibitisha kukamtwa kwa mtu huyo ambaye kwa Mujibu wa jeshi hilo mtu
huyo amekiri kuwa anajishughulisha na mtandao wa kuagiza, kuingiza na
kuhifadhi mabomu ya kivita ya kurushwa kwa mkono na mabomu hayo yalikuwa
matano na polisi wamesema huenda moja ya hilo likawa ndilo lilotumika
Darajani huku kamishna akidai mtandao huo unausishwa na matukio kadhaa.
Hata hivyo kamishna Hamdani Maka amesema kukamtwa kwa mtuhumiwa
huyo ambaye hata hivyo amekataa kumtaja jina na mazingira ya ukamataji
wake amesema hausiani na imani ya kidini na polisi inamshughulikia mtu
kisheria kutokana na kosa lake kwa mujibu wa sheria za nchi na siyo
Imani za kidini.
Wakati polisi imekataa kutoa taarifa yeyote kuhusu mtuhumiwa huyo
jeshi hilo limesema hakuna kosa lolote la kisheria endapo mtu
akipelekwa nje ya Zanzibar kwa kosa la ugaidi huku akisema bado polisi
inaendelea na upelelezi wa tukio hilo kama ni la Zanzibar au la, ama ni
mtandao wa ugaidi wa nchi nzima.