“Pole kaka yangu Chidi Benz,Naumia
kuona tatizo uliokuwa nalo bado haujalitaftia jibu unalijua la kutatua
tatizo lako,Mimi ni dada yako na tumeshafanya kazi Pamoja,Tatizo
ulilonalo na Mimi nilishakuwa nalo na niliweza kulitatua sababu
nilijitambua na kutafuta suluhu, nimejaribu kila njia kukushauri badala
yake ukaja na rungu la kimasai na kunitandika nalo nyumbani
kwangu!
nadhani janga hili lililokukuta litakuwa Kama jibu kwako kwamba
unakoenda si salama kabisa kaka yangu ni bora ubadilishe njia ili uweze
kuungana nasi kwenye tiba ya Methadone kwani ndio Kiboko ya madawa ya
kulevya!!!!
Kama Mimi mwanamke nimeweza najua Hata wewe
utaweza!!!!
Tanzania bila madawa ya kulevya Inawezekana !!
Watanzania
tusimyanyapae Msanii wetu kwani Uteja ni ugonjwa Kama ugonjwa mwingine
na Unazuilika na Kutibika,Ana kipaji na Ana uwezo wa kurudi tena kwenye
Sanaa,Tumuombee mema………Tanzania Stand Up n Wish Him Luck…………With
Like,Ray C Foundation.”