NA KENNETH
NGELESI,eddy blog KYELA
LICHA ya
Tanzania nchi na yenye rasilimali nyingi lakini ya Taifa masikini duniani na
inashindwa kupiga hatua kimaendeleo kutokana na viongozi waliopewa dhamana ya
kuingoza kujawa na ubinafsi na kwamba wakati wote wanawaza uchaguzi na siyo matatizo ya
wananchi.
Hayo
yamebanishwa juzi na Makumu mwenyekiti baraza la vijana chama cha demokrasia na
Maendeleo (Bavicha) Patric Ole Sosopi wakati akiwahutubia wananchi wa Kata
Ipinda-Kyela, katika Mkutano wa haradhara wa kukijenga chama uliofanyika katika
viwanja vya ghala la chakula mjini Ipinda.
Makamu huyo
alisema kutokana na viongozi wengi kuwa wabinafsi na muda wote wanawaza
uchaguzi, wanakosa nafasi ya kuwatumikia wananchi, na kwamba Tanzania inashindwa
kupiga hatua kutokana na watu hao waliopewa dhamani kutokuwa uchungu, bali
wengi wao ni madalali.
Sosopi
alisema, hatua pekee ya kuondoka na viongozi wa aina hii ambao aliwaita
madalali, ni kujiandikisha kwa wingi katika daftari la wakaazi ambalo lipo katika
ofisi za maafisa watendaji wa kata, na daftari na kudumu la wapiga kura ili
unapofika uchaguzi weweze kung’olewa kwa njia ya kura.
Akiwa
hutubia mamia ya wananchi wa kata hiyo Sosopi alisema kuwa kushiriki kwa wingi
katika Mikutano inayofanywa na chama hicho hakuna maana bali jukumu pekee
ni kujiandikisha katika madaftari hayo ili zinapo fika chaguzi zote, Serikali
za mitaa unao tarajiwa kufanyika Desemba mwaka huu na Uchaguzi Mkuu mwakani kuweza
kuondoa Serikali ya kidhalimu ya chama cha mapinduzi.
‘Ndugu zangu
wanaipinda na Kyela kwa ujumla, nchi hii hapigi hatua kimaendeleo kwani watu
tulio wapa dhamani si viongozi bali ni madalali ambao wanawaza familia zao tu
na ili kuondoka na watu hawa niwaombe likianza zoezi la uandikishaji katika
daftari na wakazi,mjitokeze kwa wingi ili mshiriki vyema chaguzi zote, Serikali za mitaa kwa maana ya
Wenyeviti wa vitongoji,Vijiji na Mitaa kwa mijini ili unapokuja uchaguzi Mkuu tuwang’oa hawa
madalali’ alisema Sosopi
Aidha katika
hatua nyingine Sosopi alisema kuwa viongozi wa CCM Chini ya aliye kuwa
Mwenyekiti wa Bunge maalumu la Katiba Samwel Sita kuwa itakuwa ni historia
kwani lilipofika zoezi la kupiga kura walipiga hata
marehemu hatua aliyodai kuwa haijawahi kutokea popote duniani, hivyo ni halali kwa
wafuasi wa chama cha mapinduzi kuita rasmi hiyo ni ya kihistoria.
‘Samwel Sita
na wafuasi wa chama cha Mapinduzi wanajitapa eti? katiba itakayo patikana ni
kihistoria hili ni sahihi kwani hakuna popote duniani isipo kuwa Tanzania tu
ambapo hata marehemu waliokufa wanapiga kura wakati wa kutafuta
theluthi mbili ili kuungwa mkoni’ aliongeza Sosopi
Alisema kuwa
kutokana na Serikali ya CCM chini ya Rais Kikwete kuupuza mawazo ya watanzania
yalitolewa wakati wa Tume Jaji Joseph Warioba iliyopita kukusanya maoni ya
wananchi lakini CCM imepuuza na kuamua kuweka mawazo ya kwao, alisema ni vema
wananchi hao wakakaitaa rasmi hiyo kwa kupiga kura ya hapana wakati utakapo fika wakati wa kupiga kura ndiyo ama hapana.
Mwenyekiti huyo alisema kuwa ni vema wananchi wakajenga
utamaduni wa kuiadabisha Serikali tofauti alivyo sasa ambapo badala ya Serikali
kuwaogopa wananchi ambao wameiweka madarakani lakini hali hiyo imegeuka wananchi
wanaigopa hatua ambayo ni vigumu kwa taifa kupiga hatua.
Alisema Dk Mwakyembe ni kigeugeu ni kitendo cha
waziri huyo kuyakana hata mawazo yake ambayo ni ya kitaalamu ambayo aliyafanyia
tafiti, kuwa Tanzania ilihitaji muundo wa Serikali tatu lakini ulipofika wakati
wa kujadili rasimiu iliyopendekezwa na tume ya Warioba DK Mwakyembe ameyakana,
mawazo yake jambo ambalo ni hatari kwa kiongozi na kwamba ipo siku ataweza kuwa
kana hata wananchi wake.
Aliongeza
kuwa mbali na kujipambanua kuwa anapiga vita ufisadi katika Wizara aliyo
pewa dhamana, ni vigumu kwa kiongozi huyo kufanikiwa kwani asilimia kubwa ya
watu wanafanya ufisadi na kunufaika na Wizara hiyo ndiyo wadhamini wakuu
wa chama cha Mapinduzi hiyo ni vigumu kufanikisha.
Lyata
alisema DK Mwakyembe kamwe haiwezi Wizara ya Uchukukuzi kwani katika vitengo
vyote vimeshikiliwa na wakubwa ambao kwa sehemu kubwa ndiyo wafadhili wa CCM
ambapo ndiyo inayounda Serikali anayoiongoza.
Katika
Mkutano huo ambao ulikuwa kwa ajili ya chama hicho viongozi hao wa Bavicha
kuanzia ngazi ya kata hadi taifa kwa nyakati tofauti walisema Wilaya ya Kyela
ambayo Dk Mwakyembe ni Mbunge wake haifanani na haiba aliyo nayo kwani amekuwa
akipewa sifa kama kiongozi mpiganaji lakini wananchi pamoja na mazingira kwa
ujumla hayafafani.
Akichanganua
kauli hiyo Mjumbe wa Mkutano Mkuu Taifa Joseph Kasambala alisema chama ccm kimegawanyika katika vipande vitatu ambapo
kipande cha kwanza ni kichwa ambao ni viongozi wa ngazi ya kitaifa,Tumbo ambao
ni wakuu wa Wilaya Wakuu wa Mikoa na viongozi wa chama hicho, huku kipande cha
mwisho ni Mkia ambao ni wananchi wanao yumbishwa wakiwa hawana hata mwelekeo
huku wakiendelea kujinadi na kauli hiyo.