Kipindi cha The Chart cha 100.Times Fm kinachocheza nyimbo 20 bora
kila Jumamosi kuanzia saa 4 kamili asubuhi hadi saa 6 mchana kimeanza
msimu mpya na mtangazaji mpya, Julian Ishungisa aka Jay Ree.
Jay Ree ambaye ameshafanya show hiyo tangu mwezi uliopita amekuwa
akifanya vizuri kila wiki akiwa na habari kali na mahojiano ya wasanii
wakubwa duniani kote juu ya nyimbo kubwa zinazofanya vizuri.
Kabla ya kujiunga na Times Fm, Jay Ree alikuwa akifanya kazi katika radio moja kubwa mjini Iringa.
