Watu mia moja na ishirini wamenusurika kifo na wengine kujeruhiwa
katika eneo la Kikatiti wilayani Arumeeru baada ya mabasi ya Hood
lililokuwa linatoka Arusha kwenda Iringa kugongana na basi la Isamilo
lililokuwa linatoka Moshi kuelekea mkoani Mwanza.
Wakizungumza baada ya kutokea ajali hiyo baadhi ya
mashuda na abiria waliyokuwemo katika ajali hiyo wamesema dereva wa
basi la Hood alikuwa katika saiti yake lakini ghafla lilitokea basi la
Isamilo lililokuwa linalipita Lori la mizigo kwenye kona kali pamoja na
daraja ndipo likashinda na kuingia upande wa pili.
Kwa upande wake dereva wa basi la Hood ambaye pia
ameumia mkono katika ajali hiyo amesema basi alililogongana nalo likuwa
kwenye mwendo kasi ambao ulimshinda dereva kulimudu gari hilo huku
alitoa wito kwa madereva wengine kuwa makini wanapo kuwa bara barani .
Akizungumza kwa njia ya simu kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Lebaratus Sabas amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.