Katika jicho letu mikoani Waandishi wetu Mariam Adams,Projestus
Binamungu na Silivester Bulengala wametuandalia taarifa inayojikita
katika hatari za matumizi ya mbogo za majani zisizo salama.
Huu ni moja ya mfereji wa maji machafu ambayo hutililika kutoka katika viwanda na makazi ya watu jijini Mwanza.
Pembezoni mwa mfereji huu shuguli za kilimo cha mboga mboga zinafanyika na maji haya ndio haswa hutumika katika umwagiliziaji.
Wataalamu wa afya hushauri ulaji wa mboga za majani kama moja wapo ya kiungo muhimu katika kukamilisha mlo kamili.
Mazingira yanayotumika katika uandaaji na utunzaji wa bustani kwa
baadhi ya sehemu bado ni hatari licha ya wakulima kunyosheana vidole.
Mbali na wakulima ambao hutumia maji kutoka vyanzo visivyo salama,kwa
wakulima ambao wanaendesha kilimo cha mbogamboga cha kisasa baadhi yao
wanahusishwa na matumizi holela ya dawa kwa malengo ya kujinufaisha
kifedha.
Mbali na changamoto hizo kiafya, kilimo cha mboga za
majani ni nguzo kuu kwa baadhi ya wajasiriamali hususani akina mama
katika kujikwamua na umasikini.