Drogba baada ya kurejea kundini.
Didier Drogba wakati akifanyiwa vipimo (kushoto). Kulia akisaini mkataba wa mwaka mmoja Chelsea.
Jembe ndani ya Stamford Bridge.
STRAIKA wa Ivory Coast, Didier Drogba amejiunga na klabu yake ya zamani Chelsea kwa kusaini mwaka mmoja.
Drogba mwenye umri wa miaka 36 amerejea Stamford Bridge baada ya
kuondoka klabuni hapo miaka miwili iliyopita na kwenda klabu za Shanghai
Shenua na Galatasaray.
Akiwa klabu ya Shanghai Shenua, Drogba alicheza mechi 11 na kufumania
nyavu mara 8 huku akiifungia Galatasaray mabao 15 baada ya kucheza
mechi 37.
Mkali huyo wa kucheka na nyavu anarejea Chelsea aliyoifungia mabao
100 katika mechi 226 alizoichezea tangu alipojiunga mwaka 2004 kwa pauni
milioni 24 akitokea Marseille.
Staa huyo ameeleza kuwa asingeacha fursa ya kufanya kazi na kocha wake wa zamani Jose Mourinho.
"Ilikuwa ni uamuzi rahisi - nisingeweza kuacha fursa hii ya kufanya
kazi na Jose kwa mara nyingine.
Kila mmoja anaelewa uhusiano wangu na
klabu ya Chelsea ulivyo na mara zote namekuwa nikijihis hapa ni
nyumbani" - Alisema Drogba baada ya kutua darajani.