
Tarehe 25 Julai, 2014 Alikiba ameachia single mbili mpya kwa wakati mmoja ziitwazo “Mwana” na “Kimasomaso”.
Alikiba
anajulikana ndani na nje ya Tanzania kwa hit zake kama Cinderella,
Mapenzi yanarun dunia, Single boy, na Dushelele. Cinderela ndiyo wimbo
ambao mpaka sasa umeweka rekodi ya kuuza copy nyingi katika Afrika
Mashariki mwaka 2008.
Mwaka
2012 Alikiba alishinda tuzo ya best Rhumba/ Zouk na wimbo wake wa
“Dushelele” katika tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards.
Alikiba
anajulikana kwa uwezo wake mkubwa wa kuimba na utunzi wa nyimbo pamoja
na kuwa mburudishaji mkali sana katika show zake za live na mpaka sasa
ametembea nchi nyingi sana duniani kuburudisha wapenzi wa muziki.
Sasa unaweza kupata nyimbo mbili mpya za Alikiba bure.Zipakue hapo chini