WATU WATATU WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI NJOMBE KWA TUHUMA ZA MAUAJI YA MLINZI

Jeshi la polisi mkoani Njombe linawashikilia watu watatu kwa mahojiano zaidi kuhusu mauaji ya mlinzi aliyekutwa amekufa mkoani hapo. 

Kwa mujibu wa taarifa ya polisi kwa vyombo vya habari iliyotolewa na kusainiwa na kamanda wa polisi mkoa wa Njombe SACP Fulgence Ngonyani imemtaja Bw. Abdul Kiswaga (49) mkazi wa kitongoji cha Ramadhani kata ya Njombe mjini, kuwa amekutwa akiwa ameuawa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali kichwani na mtu ama watu wasiofahamika. 

Taarifa hiyo imesema tukio hilo limetokea Juni 3 mwaka huu ambapo mwili huo wa marehemu ambaye alikuwa mlinzi umekutwa katika mtaa wa Msikitini kata ya Njombe mjini. 

Wanaokamatwa kwa maojiano kuhusu mauaji hayo ambao nao ni walinzi ni pamoja na Stephano Msasi (25) mkazi wa Uyelevale, Jacob Fungamila (22) mkazi wa Uyelevale na Julius Mwangande (55) mkazi wa Msikitini Njombe. 

Aidha mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Kibena Njombe na kiini cha mauaji hayo bado kinachunguzwa


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo