WAKATI TUKIELEKEA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI, UTUPAJI TAKA OVYO BADO NI TATIZO MAKETE MJINI

Ikiwa Juni 5 ya kila mwaka ni siku ya mazingira duniani, wilayani Makete mkoani Njombe, yapo baadhi ya maeneo yameonekana kutotunza mazingira kwa kuzagaa taka ovyo bila ya kujali athari zinazoweza kujitokeza

Mwandishi wa mtandao huu amepita katika maeneo mbalimbali ya Makete mjini na kushuhudia utupaji ovyo wa taka ilihali yapo maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya kutupa taka

Imebainika kuwa kutokana na kuwepo kwa sheria zinazowabana watu wanaotupa taka ovyo na kuchafua mazingira, wengi wa waharibufu hao wamekuwa wakitupa taka ovyo usiku kwa kuwa uwezekano wa kuonekana ni mdogo

Mmoja wa mwananchi wa kona aliyezungumza na mwandishi wetu kwa sharti la kutotaja jina, amesema kuna baadhi ya maeneo ambayo si rasmi kwa kutupa taka lakini imekuwa jambo la kawaida kwa wachafuzi hao wa mazingira kwenda kutupa taka majira ya usiku

Kwa mujibu wa idara inayohusika na mazingira kila maeneo kumekuwepo na vifaa maalum kwa ajili ya taka, na pindi zinapojaa wanatakiwa kwenda kuzitupa kwenye maeneo yaliyotengwa na mamlaka husika kwa ajili ya uteketezaji wa taka hizo


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo