Aidha, wametahadharishwa kujilinda katika kipindi cha matukio maalumu
yanayotokea nchini, ikiwemo suala la kupata Katiba Mpya na Uchaguzi Mkuu
unaotegemewa kufanyika mwaka 2015 kutotumiwa na wanasiasa na makundi
mbambali katika jamii kwa kuzingatia maadili ya kazi zao.
Wakiongea katika mafunzo yaliyoratibiwa na Mtandao wa kutetea haki za
Binadamu (Tanzania Human Rights Defenders Coalition-THRDs Coalition,
jana Juni 15, 2014 baadhi ya wahariri wa vyombo hivyo wamesema pamoja na
masuala ya usalama kuwa nyeti, matatizo yanayotokana na madhara ya
kiusalama wakati wa kutekeleza majukumu yanayoihusu jamii, pia serikali
inatakiwa kutambua umuhimu wa suala hilo ili kuondoa changamoto
zinazojitokeza.
"Maadili katika mazingira tete, katika kipindi cha uchaguzi yanatikwa
kuzingatiwa ikiwemo dhima ya maadili ya mwandishi katika taaluma ili
kuripoti masuala ya ngazi tofauti na kufanya utafiti kwa kuzingatia
taaluma ikiwemo suala la haki za binadamu" walikaririwa
Wamesema kuwa, sula la utetezi wahaki za binadamu linatakiwa kupewa
kipaumbele katika kuuhabarisha umma juu ya mambo yanayoendelea nchini,
hususani katika kipindi cha chaguzi mbalimbali ikiwemo uchaguzi mkuu
utakaofanyika mapema mwaka ujuao
Hata hivyo, wamesema kumekuwepo na tatizo la kuwepo na usiri wakutoa
taarifa ambazo wananchi wanatakiwa kuzijua, na pindi uchunguzi wataarifa
hizo unapofanywa na waandishi habari hupata vitisho na kuacha taarifa
hizo kuendelea kugubikwa na utata huku baadhi watu wakiendelea
kujinufaisha kupitia mali za umma.
Awali Mratibu wa Mtandao huo, Onesmo Olegurumwa, alisema kuwa,
mafunzo hayo yamewawezesha wahariri wa vyombo hivyo kuwa na uwezo wa
kujilinda na kutathimini athari mbalimbali kuhusu namna ya kujilinda
wawapo kazini na kujiepusha na masuala ya rushwa kwa manufaa ya
mwandishi mwenyewe na Taifa kwa ujumla.
Mafunzo.
Akifunga mafunzo hayo yaliyofanyika Juni 13-15, Katibu Mtendaji wa
Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari Nchini (Moat), Henry
Muhanika, amesema mashirika yasiyo ya kiserikali yanayoshughulikia
masuala ya utetezi, kujilinda, na kujikinga na madhara yanayosababishwa
na ukiukwaji wa haki za binadamu, mashirika hayo kwa kushirikiana na
wadau wengine wanatakiwa kutetea haki za binadamu likiwemo la wananchi
kupata haki ya kuhabarishwa kwa habari zinazowagusa moja kwa moja.
"Unapo ripoti masuala yanayomgusa mtu kwamfano amekamatwa
akijishughulisha na wizi wa meno ya Tembo ni dhahiri kuwa hamtaelewana
lakini kwa mafunzo mliyopata ninajua tumepata mbinu nyingi sana za
kujikinga mahali pa kazi" alisema Muhanika.
