WAFANYABIASHARA NDOGONDOGO MJINI NJOMBE WAHAHA SEHEMU YA KUUZIA BAADA YA HALMASHAURI KUWAFUKUZA

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgweSVlCJgGGmgvoNCogEdAhYCLm4dY2BcJHJleGStvpWa7xS1VL2iIewnt4FfguZHSYaou4DCCCJ0R63U5OIh_NWpDTqbyT21Jeegy0ZcatQgzShyphenhyphenXg6tHUXEoyI2sXOJEDl31r14DMYF9/s1600/DSC06049.JPGNa Gabriel Kilamlya Njombe
Sakata la kuwaondoa wafanyabiashara katika maeneo yao ya kufanyiabiakazi mjini njombe limendelea kushika kasi licha ya bunge kuzuia wafanyabia katika sehemu mbalimbali za miji mpaka serikali Itakapo tenga maeneo kwaajili ya kufanyia shughuli zao.

Hali hiyo imejitokea Mapema leo baada ya wafanyabiashara wanaofanyia biashara zao katika Maeneo mbalimbali Likiwemo eneo la Roman Catholiki Mjini Njombe kujikuta katika wakati mgumu baada ya uongozi wa kata ya njombe mjini kwa kushirikiana na uongozi wa mitaa mbalimbali kuambatana na Askari Polisi na Migambo Kwa lengo la Kutaka Kuwaondoa Katika Maeneo Hayo.

Zoezi hilo Limekuwa likifanyika mara kwa mara lakini wafanyabiashara hao wamekuwa wakishindwa kutekeleza agizo la kuwataka wahame katika eneo hilo ambalo ni hatari kwa usalama wao kutokana na kushinda pembezoni mwa barabara kuu ya Njombe Songea wakijishughulisha na ujasiliamali  kwa kuuza vitu mbalimbali.

sakata hilo leo Imeonekana kuwa tishio kwa wafanyabiashara hao ambao wamesema Serikali imekuwa ikiwalazimisha kuhama katika maeneo hayo ilihali hakuna maeneo shirikishi katika masuala ya kibiashara wanakooneshwa.

Kutokana na Hali Hiyo Kituo hiki kimelazimika kuwatafuta baadhi ya viongozi wa ngazi ya mitaa na kata ili kutolea ufafanuzi huo ambao Afisa mtendaji wa Kata ya Njombe Mjini Bwana Bonasius Mwalongo Amesema Kuwa Kama Serikali Haiwezi kuwaacha katika Maeneo Hayo Waendelea kufanya biashara hizo kwani ni hatari katika maisha yao na wateja wao.

Bryson Lupenza ni Afisa mtendaji wa Mitaa ya Kwivaha,National Housing na Mgendala,Mitaa ambayo imekuwa katika sakata hilo Ambaye Amesema Kuwa Amekuwa Akitoa Elimu kwa Wafanyabiashara Hao Zaidi ya mara 20 Lakini Wamekuwa Wakishindwa kutii Agizo la kuhama Katika Maeneo Hayo.

Agrey Mtambo ni Diwani wa Kata ya Njombe Mjini Ambaye Amesema Kuwa Bado Hajapokea Malalamiko hayo Lakini Ataendelea Kushughulikia Kwani Serikali inawajibu wa Kuwahamisha taratibu Mara baada ya kuwaandalia Maeneo Rafiki Katika Biashara Zao.

Wakati Bunge la Bajeti likipitisha Makisio ya Bajeti Katika Wizara ya Viwanda na Biashara Liliitaka Serikali Kuwaacha Wafanyabiashara Hao hadi pale Serikali Itakapo watengea Maeneo ya Kazi Hiyo Lakini Bado Azimio Hilo Limeonekana Kuendelea Kukiukwa na Baadhi ya Viongozi wa Mitaa na Kata.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright 2025 EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo