VURUGU kubwa zimetokea katika Viwanja vya Mwembeyanga, Temeke jijini Dar wakati wa tamasha la uzinduzi wa redio mpya ya EFM.
Vurugu hizo zilizuka wakati burudani zikiendelea baada ya
wananchi kuanza kurusha mawe na askari kuamua kutumia mabomu ya machozi
kuwatawanya.
Kutokana na vurugu hizo, tamasha halikuweza kuendelea na inadaiwa baadhi ya watu wamejeruhiwa kwenye vurugu hizo.