UJERUMANI YAICHAPA URENO YA CRISTIAN RONALDO MABAO 4-0, YAANI KAMA UNANAWA VILE....!!!

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgBlEchrQo0Cru7AAorBQe3VZjwu_jIl24E0hR-0Y2cIaKQ1gaT8KghPNoPiVpyCzwQmKRibS33LV6CtM31MH9hkUwCZJYoQdooJY99EO6B6MhXPzpnf5yGhsecvqm-tF4NaPSk0gylPkE/s1600/article-2658453-1ED2CC3300000578-228_964x356.jpgNa Sultani Kipingo

Ushindi kwa Ujerumani ulitegemewa, ukizingatia Ureno  ni kama kwamba timu ya mtu mmoja – Ronaldo. Lakini ukweli ni kwamba isingekuwa hivyo baada ya Pepe kuoneshwa kadi nyekundu katika kipindi cha kwanza. Ila mechi hii haikuwa ni juu ya Pepe, na wala haikuwa ya Miroslav Klose, na hata haikuwa juu ya Cristiano Ronaldo. Mechi yote hii ilikuwa juu ya Thomas Muller.

 Mshambuliaji huyu wa Ujerumani tayari ameshaanza mbio kuelekea kwenye mstari wa mwisho wa mfungaji bora wa michuano, baada ya kupiga mabao matatu (hat trick), na kuendelea kuinyanyasa Ureno na Ronaldo wao muda wote wa mchezo.

Hakika michuano hii ya Kombe la Dunia huko Brazil imekuwa ni ya kuvutia hadi sasa. Na mechi ya Ujerumani na Ureno ilisemwa kuwa mtanange wa mwaka. Na Ilikuwa hivyo kwa Ujerumani kuondoka na ushindi wa mabao 4-0


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo