BAADA YA NDOA YAKE KUPEPERUKA, MBUNGE VICKY KAMATA ATOA WIMBO MPYA WA MOYO WA MTU KICHAKA, USIKILIZE HAPA

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjZXhLvFsaEigGU5s_wp0QwCZnzU4zsw7oSCv9Nz6-Bh0WFCzBTkd2_BDeuqo3EbHA2Hid6TCWi9Bpa-dkD5pb9h5kthiNUCRQX4Tv3dHk4cS9VC-AAU0aRlczuC7WqHSycIiQgQEGJr3g/s1600/Vick+akikumbatiana+na+Kigwangala+(1).jpgMh. Vicky Kamata aliwasili Bungeni Dodoma na kama ilivyo ada alipokewa vizuri na kila mbunge aliyekutana nae. 

Wabunge wengi walimpa pole baada ya kuugua siku chache kabla ya ndoa yake na kumtakia kila la kheri, huku wengi wakiamini kilichotokea ni mpango wa Mungu na kua Ndoa yake ipo na itakuwepo siku yoyote Mungu akiamua kulitimiza kusudi lake juu ya Mh. Vicky Kamata.. 

 Wakati wabunge wengi wakimuhurumia na kudhani kua kutofungwa kwa ndoa yake kungemgharimu siku nyingi kurudi katika hali ya kawaida, 

lakini  ilikua ni tofauti kabisa kwa upande wa Mh. Vicky Kamata kwani muda wote alikua na amani na kwamba hakujiskia vibaya kama wengi walivyodhani na ndio maana ilichukua muda mfupi sana na aliweza fika Bungeni na kazi ya kuwatumikia wananchi wake wa Geita na Tanzania kwa ujumla ilianza mara moja na kwamba bado anaamini kilichotokea ni mpango wa Mungu na kwamba Mungu hakosei na anamini Muda si mrefu atafunga ndoa na kila mtu atashuhudia na mkono wa Mungu utasiamama juu ya ndoa yake.
Na anabainisha yote hayo katika wimbo wake mpya "Moyo wa mtu Kichaka" hapo chini. (Picha kwa hisani ya Vicky Kamata blog)


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo