Mgeni
Rasmi kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma Waziri wa Nchi
Ofisi ya Rais Utawala Bora Kapteni Mstaafu George Mkuchika akizungumza
kuzindua Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma iliyoanza leo kwenye
viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salam.
=======
Hussein
Makame-MAELEZO
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Utawala
Bora, Kapteni Mstaafu George Mkuchika amesema kuwa Tanzania inashika nafasi ya
pili kati ya nchi tano za Shirikisho la Afrika Mashariki katika suala la
Utawala Bora na vita dhidi ya Rushwa.
Waziri Mkuchika amayasema hayo wakati
akizindua Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma iliyoanza leo kwenye viwanja
vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Alisema kuwa tangu Serikali ya Awamu ya
Kwanza, Serikali ya Tanzania ilitangaza vita dhidi ya Rushwa na imekuwa
ikiimarisha mapambano dhidi ya adui huyo hadi katika Serikali ya Awamu ya Nne
chini ya Rais Jakaya Kikwete.
“Katika nchi za Afrika Mashariki suala
la Utawala Bora na Vita dhidi ya Rushwa, Tanzania tunashika nafasi ya pili,
Rwanda ni ya kwanza, ya tatu ni Uganda na ya nne ni Kenya” alisema Waziri
Mkuchika. Waziri Mkuchika alikuwa akizungumzia
madai yanayotolewa na baadhi ya watu hapa nchini kuwa Serikali ya Tanzania
haina dhamira ya kupambana na Rushwa.
Alikanusha madai hayo na kusema kuwa
Serikali ya Tanzania ina dhamira ya kupambana na Rushwa ndio maana imepitisha
Sheria dhidi ya Rushwa,Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini
(Takukuru) ina matawi kila mkoa na kila wilaya.
Alisema
kiashiria kingine cha kuthibitisha kuwa Serikali ya Tanzania inapamabana
na Rushwa ni kufikishwa mahakamani kwa watu wanaotuhumiwa na Rushwa. Hata hivyo, alibainisha kuwa mtumishi wa
Takukuru hawezi kuwafikisha watu mahakamani bila ya kupata taarifa kutoka kwa
wananchi.
Hivyo aliwataka Watanzania wote kutambua
kuwa wana wajibu wa kupambana na rushwa kwa kutoa taarifa kwa mamlaka husika
ili kufanikisha vita hiyo dhidi ya Rushwa. Waziri Mkuchika aliwakumbusha Watanzania
kuwa mtumishi yeyote wa umma kumhudumia mwananchi ni haki yake, hivyo mtumishi
anayeomba Rushwa ili atoe huduma anashiriki katika tendo la Rushwa. Kutokana na hali hiyo, aliwaomba
watumishi wajiepushe na Rushwa kwani Rushwa inawanyima watu haki, kukiwa na malalamiko
anayepata haki ni yule anayetoa Rushwa.
Kaulimbiu ya Maadhimisho ya Wiki ya
Utumishi wa Umma ya mwaka huu inasema “Mkataba wa Misingi na Kanuni za Utumishi
wa Umma Barani Afrika ni Chachu ya Kuimarisha Utawala Bora na Uendeshaji wa
Shughuli za Serikali kwa Uwazi”.
Naibu
Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma Hab Mkwizu
akizungumza wakati akimkaribisha Mgeni Rasmi kwenye Maadhimisho ya Wiki
ya Utumishi wa Umma iliyoanza leo kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini
Dar es Salam.
Baadhi
ya watumishi wa Umma wakifuatilia Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa
Umma yaliyoanza leo kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salam.
Brass
Band ya Jeshi la Polisi ikiongoza maandamano ya Maadhimishi ya Wiki ya
Utumishi wa Umma iliyoanza leo kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar
es Salam.
Watumishi
kutoka Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa wakipita mbele ya
meza Kuu wakati wa Maandamano Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma
yaliyoanza leo kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salam.
Afisa
Habari wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Robi Bwiru
akimueleza jambo mmoja wa wananchi waliotembelea banda la Wizara hiyo
wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma iliyoanza leo kwenye
viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salam.
Baadhi
ya wananchi wakipata maelezo kuhusu shughuli zinazofanywa na Wizara ya
Ushirikiano wa Afrika Mashariki , wakati walipotembelea banda la Wizara
hiyo.
Picha na Hussein Makame-MAELEZO .