MAJONZI TENA KENYA, MASHAMBULIZI YA AL SHABAAB YAUA WATU 48



WATU 48 wameripotiwa kuuawa, hoteli mbili, kituo cha polisi na kituo cha mafuta kuchomwa moto baada ya shambulio lililotokea eneo la Mpeketoni, Lamu nchini Kenya jana usiku.
 
Kituo cha Polisi cha Mpeketoni, hoteli ya Breeze View na Taweel ndivyo vilivyochomwa moto na moshi ulikuwa bado unafuka leo  asubuhi .
 
Imeelezwa kuwa washambuliaji walitokomea na silaha na magari ya polisi kutoka kutuo hicho cha polisi baada ya kushambulia.
 
Awali washambuliaji hao waliteka daladala mbili 'matatu' eneo la Witu kabla ya kufanya shambulio hilo.
 
Wananchi walikimbilia katika nyumba zao wakati polisi wakijibizana risasi na magaidi hao ambapo mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo anadai kusikia washambuliaji hao wakisema "ambieni baba yenu atoe jeshi Somalia” wakimaanisha wamwambie Rais Kenyatta aondoe jeshi nchini Somalia.
 
Makundi ya Al Shabaab na MRC militia yanadaiwa kuhusika na shambulio hilo
 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo