ALIYEWAHI kuwa Katibu Mkuu wa Dar es salaam Young Africans George
Johnson Mpondela ‘Castor’ amefariki dunia jana saa nne usiku katika
hospitali ya Muhimbili, Dar es Salaam alikokuwa amelazwa kwa matibabu ya
moyo.
Mtoto wa Marehemu Bwana Hilton amesema kwamba baba yake
aliyekuwa akiishi eneo la Machava, Kigamboni, Dar es Salaam amekuwa
akisumbuliwa na maradhi ya moyo kwa miaka minne sasa.
Amesema msiba uko nyumbani kwao, eneo la Karakata, Uwanja wa Ndege karibu na Kanisa Katoliki na kituo kidogo cha Polisi, maarufu Polisi Posti.
Marehemu ameacha mke na watoto tisa, ambao ni Pius, Robert, Hilton,
Kennedy, Joseph, Collin, na wa kike Linda, Jaqcueline na Jennifer.
Hilton amesema mwili wa marehemu utasafirishwa Jumanne kwenda Tabora baada ya kuagwa kuanzia Saa 2:00 asubuhi hospitali ya Muhimbili tayari kwa mazishi yake Jumatano kijiji cha Misha wilaya ya Tabora vijijini.