Aidha, Mtoto mwingine mwenye umri wa miaka kumi na tatu mfanyakazi wa
ndani na mkazi wa Majengo Wilayani Moshi, mkoani humo amebakwa na
kuumizwa vibaya katika sehemu za siri na, Rajabu Hamza(18), Kinyozi
mkazi wa Njoro.
Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani humo, Koka Moita, amesema kuwa
tukio hilo lilitokea Juni 12, 2014 saa moja jioni katika mtaa wa
Majengo Wilayani Moshi, baada ya Rajabu, kumshawishi msichana huyo kuwa
amfuate katika nyumbani aliyopanga rafiki wa mtuhumiwa 'geto' ndipo
alipoamua kumbaka wakati akijua kufanya hivyo ni kosa kisheria.
“Kwa sasa tunashindwa kuelewa ni kwanini matukio ya ubakaji kwa hawa
watoto wa kike yameshika kasi kipindi hiki, kwani itakumbukwa ndani ya
wiki karibia tatu wameshabakwa watoto watatu, ambapo wawili kati ya hao
wamebakwa na baba zao wazazi” alisema Moita.
Amesema kuwa Jeshi la polisi mkoani humo linamshikilia mtuhumiwa huyo
kwa mahojiano zaidi na pindi ushahidi utakapo kamilika mtuhumiwa
atafikishwa mahakamani.
Amewataka wazazi na walezi, kuwa makini na uangalizi mkubwa kwa watoto
wao, na kuepuka kuwaachia ovyo watoto wao kwa watu mbalimbali na kuwa na
ukaribu na watoto hao.
Katika tukio jingine mtu mmoja amekufa kwa kujinyonga ndani ya chumba
chake katika kijiji cha Kiboroloni-Makao mapya Wilayani Moshi, mkoani
humo.
Moita, amesema tukio hilo lilitokea Juni 12, 2014 saa 12:00 mchana na kumtaja marehemu kuwa ni, Izaki John (30).
“Tulimkuta akiwa amejinyonga kwa kutumia Mkanda wake wa suruali na
alikuwa ameshakufa, ndipo Polisi wetu walimtoa na kumchukua kwa ajili ya
uchunguzi" alisema Moita.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya mkoa ya Mawezi, kwa
uchunguzi zaidi, huku Jeshi la hilo likiendelea na upelelezi ili kujua
chanzo cha marehemu kuamua kujinyonga.
