Tukio la aina yake ambalo limeonekana kuwashangaza wengi limetokea kwenye mataa ya kuongozea magari jijini dar es Salaam ambapo askari wa usalama barabarani ameamua kusimama mbele ya magari yaliyokaidi amri yake ya kuzuia magari ya upande huo yasipite kwanza
Tukio hilo limetokea mwishoni mwa wiki ambapo askari huyo ambaye jinalake halikupatikana mara moja aliamua kuyazuia magari mawili toyota baloon yaliyokaidi amri yake aliyoitoa kuwa magari ya upande huo yasimame ili aite magari ya upande mwingine
Wakati askari huyo alipotoa amri ya kuzuia magari yaliyokuwa yakitoka mjini kwenda mbezi na maeneo mengine ya nje ya mji, aligeuka upande wa pili kuita mengine lakini ghafla madereva hao wakataka kutumia mwanya huo wa kugeuka kwa askari kupenya
Jambo hilo lilionekana kumkera askari huyo ambaye alitoa ishara ya kuzuia magari yote kupita kwa muda halafu akasimama mbele ya magari hayo yaliyotaka kupita kwa nguvu huku akiwaambia kama wao ni madereva wamgonge wapite
Kitendo hicho kilichochukua zaidi ya dakika 5 kilionekana kuwashangaza wengi na pia madereva hao walishindwa kupita na kulazimika kutii amri ya polisi huyo ya kuwataka warudishe magari yao nyuma na kusubiri kwenye foleni hadi hapo upande wao utakapoitwa