WANANCHI WAMPIGA NA KISHA KUMCHOMA MOTO KIJANA MMOJA ALIYETUHUMIWA KUIBA NG'OMBE MBEYA.

WAKATI vyombo mbali mbali zikiendelea na jitihada za kuwaelimisha wananchi juu ya madhara ya kujichukulia sheria mkononi hali hiyo bado ni tete mkoani Mbeya.
 
Hali hiyo imezidi kujitokeza baada ya Wananchi wa Mwasanga Ivumwe jijini Mbeya kumpiga na kumchoma moto mwananchi mmoja ambaye jina lake halikupatikana mara moja wakimtuhumu kwa Wizi wa Ng’ombe mmoja na ndama.
 
Kwa mujibu wa shuhuda wa tukio hilo ameuambia mtandao huu kuwa tukio hilo lilitokea mapema leo asubuhi ambapo chanzo ni wizi wa Ng’ombe wa Kongoro Mwakitalima mkazi wa Isyesye kata ya Ilomba.
 
Alisema Ng’ombe huyo aliibiwa jana majira ya usiku ambapo mzee huyo alitoa taarifa kwa majirani ambao asubuhi walijihimu kutafuta ambapo walipofika maeneo ya  Ivumwe walikutana na mwendesha boda boda ambaye aliwaambia amekutana na mtu akiwa anaswaga hiyo mifugo.
 
Alisema baada ya kusikia hivyo waliamua kuanza kumfukuzia wakitumia bodaboda na ndipo walipofika eneo la Mwasanga relini walimkuta mtuhumiwa akiwa na hao Ng’ombe.
 
Alisema Wananchi mbali mbali walikusanyika na kuanza kumshushia kipigo kutokana na eneo hilo kukithiri kwa wizi wa mifugo lakini baada ya kipigo hicho mtuhumiwa alionekana kuwa ngangari jambo lililowatia hasira na kuamua kumchoma moto.
 
Shuhuda huyo aliendelea kusema baada ya kuanza  kumchoma lakini katika hali isiyokuwa ya kawaida mtu huyo hakuweza kukata roho hadi alipookolewa na Askari wa jeshi la polisi walipofika eneo la tukio.
 
Hadi tunaingia mtamboni hakuna taarifa zilizothibitisha kama mtuhumiwa huyo bado yuko hai ama amepoteza maisha.
 
>>>>MBEYA YETU


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright 2025 EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo