Mgeni
ambaye ni mwenyekiti wa ccm mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu
akizungumza na wazazi na wanafunzi wa shule ya shule ya sekondari ya
wasichana Iringa katika ukumbi wa shule hiyo hivi karibuni.
Baadhi ya wahitimu wa kidato cha sita wa shule ya sekondari ya wasichana wakiwa katika mahafali yao
=======
Na Denis Mlowe,Iringa
WANAFUNZI
wa kike wanaotarajiwa kuhitimu elimu ya kidato cha sita wameaswa
kujiamini,kujitambua na kufahamu wajibu wao kwa jamii inayowazunguka kwa
kutokukimbilia kuolewa kwa lengo la kujikomboa kifikra na kiuchumi na
kutimiza ndoto za maisha yao.
Ushauri
huo ulitolewa mwishoni mwa wiki na mgeni rasmi Mwenyekiti wa Chama cha
Mapinduzi (CCM) mkoa wa Iringa, Jesca Msambavangu,wakati wa harambee na
mahafali ya 22 ya shule ya sekondari ya wasichana ya Iringa na kufanyika
katika ukumbi wa shule hiyo mjini hapa.
Msambavangu
alisema imeibuka kasumba kwa wanaume wengi kukimbilia kwa wasichana
wadogo na kuwaharibia maisha yao kabla hawajatimiza ndoto zao za maisha
kutokana na kupewa ujauzito na wanaume wenye nia mbaya na maisha ya
mabinti.
Alisema
ndoto nyingi za wasichana zinakatishwa na wanaume wakware na wasichana
wengi wanamalengo ambayo wanataka kutimiza lakini kutokana na mabadiliko
ya haraka kwa watoto wa kike yanaweza kukuletea madhara kuliko faida na
kuwataka kukazania masomo.
“Asilimia
kubwa ya wazazi wanataka mtoto wao asome afikie ngazi kubwa kama baadhi
ya viongozi wa kike waliomadarakani lakini kwa tamaa za chips kuku
wengi wenu mmekuwa mkiishia njiani, nawaomba sana watoto wangu msiende
njia ambayo wakware watawadanganya na kuzimisha ndoto zenu za kuwa
madaktari, walimu na viongozi wa baadaye someni sana” aliwaasa
Msambavangu.
Amewataka
wanafunzi hao kutambua thamani yao kuepuka kutumiwa vibaya na kushinda
majaribu ya watu wanaotaka kuwavurugia safari ya maisha waliyoanza nayo
tangu wakiwa wadogo kwa kuwakataa wanaume wenye fedha na wasiona fedha
kwa kuongwa vitu vidogo vidogo vikiwemo simu na nguo.
Aidha
aliwataka kuacha tabia ya wanafunzi kuchukua muda wao mwingi kwenye
mitandao ya kijamii kwa kufuatilia mambo yasiyo na msingi kwao na badala
yake watumie mitandao hiyo kwa manufaa yao kielimu.
Katika
harambee ya kuchangia ununuzi wa gari la shule Msambatavangu alichangia
shilingi milioni 1.5 na kiasi kilichopatikana kilikuwa shilingi milioni
4 .6 kati ya shilingi milioni 25 zinazohitajika.
Awali
mkuu wa shule hiyo Joyce Msigwa aliwashukuru wazazi wa wanafunzi kwa
michango yao na kuongeza kuwa kuna changamoto kubwa ya usafiri wa
wanafunzi katika shule hiyo na wanatarajia kukusanya fedha hiyo kuweza
kuondokana na hali hiyo na kuwatakawadau kuwachangia kiasi cha fedha
kilichobaki.
Alisema
kuwa wanafunzi wanakabiliwa na wakati mgumu inapojitokeza dharula
katika kutekeleza majukumu ya shule na wanafunzi wanapohitaji gari
wakipatwa na matatizo hususani katika kipindi cha ugonjwa.
“Tunaomba
wadau mbalimbali, wazazi na makampuni mbalimbali kutuchangia katika
ununuzi wa gari la wanafunzi ambalo bei yake ni kubwa hivyo tunategemea
sana misaada kutoka kwao na waandishi tunaomba sana mtusaidie kufikisha
ujumbe kwa jamii kuweza kuwakomboa hawa mabinti wawe na usafiri wao
yaliyokuwepo yote yameharibika” alisema Msigwa