Sakata la baadhi ya wabunge kutuhumiana kuwa wamechukua fedha za
serikali kwa ajili ya kufanya Safari na hawakusafiri limechukua sura
nyingine baada ya spika wa bunge Mh. Anne Makinda kuwataka wale wote
waliochukua fedha hiizo bila ya kusafiri wazirudishe na huku akisisitiza
anawajua wote kwa majina.
Mh Makinda ameyasema hayo alipokuwa akiongoza
mkutano wa kumi na nne na kikao cha kumi na tisa ambapo amesema
anashangazwa na maneno maneno ambayo wabunge wamekuwa wakitupiana
wakati anawajua wote waliochukua fedha bila ya kusafiri.
