MSANII maarufu wa muziki wa kizazi kipya anayeendelea kukubalika
katika tasnia hiyo, Naseeb Abdul au maarufu kwa jina la Diamond Platinum
sasa amembadili jina mpenzi wake waliyerudiana hivi karibuni msanii wa
kuigiza filamu, Wema Sepetu.
Diamond alijikuta akimbadili jina mpenzi wake bila kutegemea baada ya
juzi usiku kujishindia tuzo saba katika vipengele tofauti
alivyoshindanishwa kwenye Shindano la Tuzo za Muziki, maarufu kama "Kilimanjaro Tanzania Music Award" (KTMA).
Baada ya tukio hilo la ushindi wa tuzo, Wema Sepetu mpenzi wa Diamond
sasa amebatizwa jina na kuitwa MRS MI-AWARDS jina alilopewa na staa
mwenzake wa filamu, Elizabeth Michael a.k.a Lulu baada ya mpeziwe kutwaa
tuzo kibao.
Lulu alimpa jina hilo Wema baada ya kuandika kwenye mtandao kuwa
anapenda ambadili jina Wema na kuitwa Mrs Mi-Awards kuanzia sasa. "Naomba kuanzia leo nikiite MRS MI AWARDS kha tuachane na jina jipya
bi dada" aliandika Lulu kwenye ukurasa wake wa instagram juzi.
Diamond alishinda tuzo zote saba alizoshindanishwa na kuweka historia
katika shindano la KTMA. Tuzo saba alizonyakuwa Diamond juzi ni ya Wimbo
Bora wa Pop, Mwimbaji Bora wa Kiume wa Kizazi Kipya, Msanii Bora wa
Kushirikishwa/Kushirikiana, Mtunzi Bora wa Mwaka wa Kikazi Kipya, Video
Bora ya Mwaka, Wimbo Bora wa Mwaka na Mtumbuizaji Bora wa Kiume.
Katika
vipengele hivyo Diamond alifanikiwa kutwaa tuzo zote saba na kuwabwaga
washindani wake.
Katika hafla hiyo moja ya tuzo hizo alikabidhiwa na mpenzi wake, Wema
Sepetu ambaye alionekana kufuraishwa zaidi na mafanikio ya rafiki yake
huyo ambaye amerudiana kimapenzi hivi karibuni na kuonesha mapenzi motomoto.
Na Mwandishi Wetu, Thehabari.com Dar
