Kamishna wa Polisi Jamii Tanzania Mussa Ali Mussa, amewataka
wafanyabiashara wadogo (Machinga) na Bodaboda Jijini Mwanza kutokubali
kutumiwa na baadhi ya makundi ya watu wanao jihusisha na uhalifu.
Mwezi Mei 27 katika eneo la Makoroboi,
Kamishina Ali, alieleza kwamba, yapo baadhi ya makundi ya wahalifu
ambayo hayana nia njema kwa watanzania badala yake yanakuwepo kwa ajili
ya kuwakosesha amani wananchi na kusababisha vurugu zisizo na manufaa
yoyote katika jamii.
“Baadhi ya makundi kazi yake ni uhalifu, hivyo msikubali kutumiwa na
hayo makundi kwani hayana nia njema na sisi kutokana na kuona kuwa tuna
kipato kidogo na endapo tukijihusisha nao tutajitoa katika dhima njema
tuliyo kusudia”, alisema Kamishina .
Alieleza kwamba kutokana na makundi hayo ya Machinga na Bodaboda,
kuna uwezekano mkubwa wa watu waovu kujiingiza katikati yao na kuwataka
kuwapa pesa katika kuwabaini watu hao mapema iwezekanavyo.
“Bodaboda nyingi hutumiwa na wahalifu kwa ajili ya wizi, cha msingi
ni kuwatambua mapema ili msijiharibie sifa zenu za uendeshaji kwani
jeshi la polisi lina mkakati wa kuwawekea mazingira safi ya kazi ili
kuepukana na ajali za mara kwa mara”, alieleza.
Kamishina Ali, alikabidhi pikipiki 13 zenye thamani ya sh.milion
mbili, ambazo zilipatikana kutoka kwa madereva pikipiki wa kituo cha
Tanesco ambao walikuwa wakichangia sh. 5,000 kila siku kwa kila mmoja na
hivyo kujipatia pikipiki hizo ambazo ni msaada mkubwa kwao katika
utendaji wa kazi.