AJALI MBAYA YATOKEA MWEKA MOSHI VIJIJINI, YAHUSISHA VX NA DALADALA

Ajali imehusisha gari ya abiria aina ya hiace inayofanya safari zake kati ya Mweka na moshi mjini  na landcruiser VX iliyokuwa  imewabeba  wanafunzi wa chuo cha usimamizi na uhifadhi wa wanyama pori Mweka kilichopo Mweka, Moshi vijijini. 
 
Kwa mujibu wa shuhuda wa ajali hiyobwana Fred Mushi amesema kuwa gari aina ya landcruiser VX iligonga daladala  hiyo  iliyo kuwa imesimama kupakia abiria kwenye kituo kimoja maarufu kwa jina la Kona. 
 
Ajali hiyo imetokea muda wa saa 10.30 jioni
Gari aina ya landcruiser VX iliyokuwa na wanafunzi toka chuo cha Mweka ikiwa imezama kwenye mtaro  na kuharibika vibaya baada ya ajali hiyo mbaya iliyotokea jioni hii
mashuhuda walikokuwa eneo la tukio wakilitazama gari aina ya landcuriser iliyokuwa imezama kwenye mtaro baada ya ajali hiyo iliyotokea jioni hii na kusababisha majeruhi
daladala iliyogongwa vibaya na landcuriser ikiwa imeharibika vibaya ubavuni kiasi cha kutoweza kutembea tena lakini Taarifa za awali hali ya dereva wake   inasemekana kuwa mbaya pia idadi ya majeruhi mpaka tunaenda mitamboni  haijajulikana.

tutaendelea kukujuza jinsi taarifa zitakavyofikia kuhusu hali na idadi Ya majeruhi.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo