KITUO CHA DALADALA UBUNGO CHAGEUZWA SOKO

 Mfanya biashara akipanga bidhaa zake tayari kwa biashara.
 Wafanyabiashara wakipanga bidhaa zao.
 Mwana baba naye akipanga sawa vitunguu kwa ajili ya kuviuza
 Huyu akisogeza mchanga uliowekwa kituoni humo kwa ajili ya shughuli za ujenzi wa barabara ili apate sehemu ya kupanga bidhaa zake.

Kilichokuwa kituo cha daladala cha Ubungo jijini dar jirani na Tanesco ambacho kwa sasa hakitumiki kwa daladala kutokana na ujenzi wa barabara ya magari yaendayo haraka, kwa sasa kimegeuzwa kama soko kwa wafanyabiashara wadogowadogo jijini hapo

Mtandao huu umeshuhudia wafanyabiashara wakiwa "bize" na shughuli zao za biashara huku wengine wakijiandaa kuweka bidhaa zao

Ikumbukwe kuwa jiji la Jiji la Dar lilishapiga marufuku wafanyabiashara kufanya biashara katika eneo hili siku kadhaa zilizopita Lakini si unajua tena maisha ni magumu hivyo wanajitafutia fedha za kujikimu na maisha.

Picha/Habari na Eddy Blog


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo