Kundi
la mbwa wenye kichaa limezuka katika Mtaa wa Swaswa Manispaa ya Dodoma
na kusababisha hali ya taharuki baada ya kuwangata watu wawili na
kuwasasabishia maamuvu makali.
Akizungumza
nasi mzazi wa mmoja wa mtoto alieng’atwa na mbwa hao Bw
Jonathani Ngossi amesema kuwa mbwa hao wamekuwa wakiwang’ata watu
wazima na watoto hivyo kupelekea kutibiwa kwa gharama kubwa.
Aidha
Bw Ngossi imeitaka serikali kwenda kutoa chanjo kwa mbwa hao ili
kupunguza tatizo hilo na kama ikishindikana iwapige risasi mbwa hao.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Mtaa huo Bw Chales Nyuma amekiri kuwepo kwa
tatizo hilo na kusema kuwa mpaka sasa watu wawili pamoja na kuku wawili
wameshang’atwa na mbwa hao na wanaendelea kutishia amani mtaani hapo
Sanjari
na hayo Bwana Nyuma ameongezea kuwa kwa baadae wanakusudia kutoa
elimu kwa watu wenye mbwa juu ya taratibu za kuwafuga.
