Mtoto mwenye ulemavu wa akili wilayani Korogwe, mwenye umri wa miaka
15, amefungiwa chumbani na mama yake wa kambo kwa muda wa miaka 9,
ambapo amekuwa akijisaidia humo choo kikubwa na kidogo, kisha kuwekewa
chakula katika bakuli lake maalum ndani ya chumba hicho
Mwandishi
wetu ameshuhudia mtoto huyo akiwa chumbani na upande mmoja wa kanga
huku kukiwa na vinyesi na bakuli lake analowekewa chakula mithili ya
mnyama.
Mama mlezi wa mtoto huyo
mlemavu aliyejulikana kwa jina la Khadija Makame alipoulizwa kuhusu
kitendo cha kumfungia ndani mtoto huyo, amesema kuwa huwa anamtoa nje
kwa chakula na hata kumsindikiza chooni, majibu ambayo majirani
walipingana naye baada ya kushuhudia ndani ya chumba chake kukiwa na
vinyesi na bakuli lake la kulia
